1985 - 2007


2. Habari Njema

Support Pages   Index To All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index

 

 Soma Haya Katika Biblia Yako

1 Wakorintho 15:1-34; 15:58

 

Mstari wa Kukariri

“Kwa maana siionei haya injili, kwa sababu ni uweza wa Mungu uletao wokovu, kwa kila aaminiye…”  Warumi 1:16.

 

Baadaye Tafakari Kuhusu Jambo Hili

Je, umeshatubu dhambi zako na kumpokea Yesu kuwa Mwokozi wako?  Ikiwa bado, huu ndio wakati mwafaka wa kufanya hivyo.

 

Jambo la Kufanya Kabla Hatujakutana Tena

Jiamulie mwenyewe ni wasioamini wangapi utakaowapelekea habari hizo kuu.  Je ni mmoja, wawili, wanne au zaidi?  Usivuke kiwango cha imani yako, lakini weka lengo na umwombe Mungu akuwezeshe.

 

Kazi ya Kuandika ya Stashahada

Andaa mahubiri ya kurasa mbili kuhusu somo utakalochagua mwenyewe, lakini pia uhusishe vipengele vya maarifa uliyoyapata kutokana na somo hili la Injili.

 

Tafakari Mistari Ifuatayo, Neno Kwa Neno

Mithali 30:2-4

 

Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu

 

Ombea Taifa La Mauritania

Idadi ya Watu ni 2,500,000

Watu Wasiomjua Yesu ni 99.7%

 

 

Hakikisha umewafundisha wengine somo hili.
Kila mara omba na kujiandaa ukiongezea mistari mingine ya Biblia
na mifano yako mwenyewe ili kufanya somo lieleweke vizuri zaidi.
 

 

(1) Je, Waweza Kusikia Swali?

 Je, waweza kusikia rohoni mwako kilio cha moyo mtulivu ukiulilia ulimwengu wa vatu?  Hebu sikiliza.

 

Nimechoka ee Mungu

Nimechoka ee Mungu, na kuzimia

Mimi ni mjinga kuliko watu wote

Sina ufahamu wa kibinadamu

Sijajifunza hekima, wala sina maarifa kumhusu Yeye Aliye Mtakatifu

Je, ni nani aliyepaa mbinguni na kushuka tena chini?

Je, ni nani aliyeukusanya upepo mikononi mwake?

Je, ni nani aliyeyafungia maji katika vazi lake?

Na je, ni nani aliyefanya imara miisho yote ya dunia?

 

Jina lake ni nani?

Na mwanaye jina lake nani?

Niambie kama unajua!

(Mit 30:1-4)

 

Mamilioni ya watu wamechanganyikiwa kwa kutokujua maana halisi ya maisha. Hawajui walikotokea, ni kwa nini wapo hapa, na ni wapi watakwenda maisha yanapofikia ukomo.  Mioyoni mwao wanahisi yupo Mungu, lakini ni nani huyo Mungu, anakaa wapi, na anafananaje?  Wewe unamfahamu huyo Mungu, na jina la Mwanaye unalijua, ni Bwana wetu Yesu Kristo. 

(2) Tumwambie Nini?

 Katika kujibu swali hilo, Paulo aliwaandikia rafiki zake kwenye kanisa lililokuwa Korintho huko Ugiriki. Alisema kuna mambo sita muhimu ambayo watu wanapaswa kuyajua ili waweze kufanya maamuzi sahihi kuhusu lile watakalo kulifanya 
(1Kor 15:1-28).
 

o        Kuna ujumbe kutoka kwa Mungu

o        Yesu aliyekufa, amefufuka na yu hai

o        Kuna neema na fadhila kutoka kwa Mungu

o        Kifo si mwisho

o        Yesu Kristo anakuja tena

o        Kutakuwa na siku ya mwisho

(3) Mwambie Anaweza Kumjua Mungu

 Biblia inasema kuwa, “ ni jambo la umuhimu wa kwanza” kwamba kila mtu, awe mwanamume au mwanamke, mvulana au msichana, kila mtu aisikie Injili, ambayo ni ujumbe unaomwunganisha tena mwanadamu na Mungu.

 

Je, Hiyo Injili Ni Nini?

Ni uweza wa Mungu kwa kila aaminiye (Rum 1:16).  Paulo anatuambia kwamba Kristo, mwana wa Mungu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, akazikwa, na siku ya tatu akafufuka (1Kor 15:1-4).

 

1.    Lazima tuamini kwamba Mungu yupo, na Yeye ndiye anayewakirimia wote wamtafutao kwa  bidii. Yeye si katili, wala hayupo mbali (Ebr 11:6).
 

2.    Ni lazima tuamini kwamba Yeye ni Mungu Mtakatifu, na ya kwamba dhambi zetu nyingi; za kutokumtafuta Yeye, na kujiendea njia zetu wenyewe, mawazo mabaya, maneno mabaya na matendo mabaya; zote hizo zimetutenganisha sisi mbali na upendo wa Mungu na uwepo wake. Matokeo yake ni kwamba baada ya kifo ni adhabu ya kutisha (  Rum 3:23; 6:23).
 

3.    Tunachagua kuamini kwamba Mungu katika upendo wake mkuu alimtuma Mwanaye Yesu, akazaliwa na bikira, katika hali ya kutokuwa na dhambi, ili atunusuru kwa kuichukua asirá ya haki ya Mungu, ili kwamba tuweze kuwa na amani na Mungu, na pia tuweze kupaingia patakatifu pake sasa na katika kufa kwetu (1Pet 2:24,25).
 

4.    Tunaamini kuwa ni wajibu wetu kufanya mwitikio sahihi. Tunakubali kwamba tumetenda dhambi na kwa kweli tunajuta sana kwa hali hiyo. Tunaamini kwamba Yesu alikufa kwa ajili yetu, na sasa tunamwomba Mungu atuwezeshe kuacha uovu.  Tunampokea Yesu kuwa Mwokozi na Bwana, na kuahidi kumfuata Yeye situ zote hata kama rafiki na jamaa wataleta shida (Yn 1:12,13) (Ufu 3:20). 

(4) Mwambie Kwamba Yesu Yu Hai

 Imani yetu haikujengwa juu ya hisia tu, bali imesimama kwenye kweli zinazoweza kukubalika na mahakama yo yote kama vielelezo muhimu vya ushahidi. Paulo anaandika ushuhuda wa watu 514 ambao walishuhudia kwa macho yao; ambao ni pamoja na wale waliotoa taarifa za Yeso kwa sababu walimfahamu vizuri. Hao ni kama Petro na wale mitume wengine, ambao kwa vyo vyote wasingeweza kufanya mañosa katika kumtambua Bwana (1Kor 15:5-8). 

(5) Mwambie Kwamba Neema Ipo Kwa Ajili Yake

 Neema ni haki asiyostahili mtu, anayoipokea bure kutoka kwa Mungu. Hainunuliwi wala haipatikani kwa malipo; inapokelewa tu kwa shukrani. Paulo anasema, ingawa alilitesa kanisa, hata hivyo neema ya Mungu imefanya kazi kwa nguvu maishani mwake.  Neema ya Mungu ilimwinua Paulo kutoka katika kuwa mkuu wa wenye dhambi, na kuwa mtu wa Mungu mwenye uwezo mkubwa (1Kor 15:9,10). 

(6) Mwambie Kwamba Kifo Si Mwisho

 Ni hapo tu tutakapokuwa tumemchagua kumfuata Yesu, Edipo hapo tutakapoweza kuingia katika uwepo wa Bwana situ ya kufa kwetu.  Tunatarajia ufufuo ujao ambapo waamini watavikwa miili mipya isiyozeeka, isiyougua wala kufa. Tutaishi kwenye dunia mpya na chini ya mbingu mpya. Lakini wasioamini watarajie tu ziwa la moto na mateso yasiyokoma mbali na upendo wa Mungu (1 Kor 15:12-23, 35-49). 

(7) Mwambie Yesu Anakaribia Kurudi

 Atakapokuja ataleta haki kwa watu wote hapa duniani, tukiamini ahadi ya malaika katika Matendo 1:11, na ya wakristo wa vizazi vyote hadi kufikia leo (1 Kor 15:23,25). 

(8) Mwambie Kwamba Kuna Siku Ya Mwisho

 Leo ndiyo siku ya kupokea wokovu wa Mungu; na sasa ndiyo wakati mzuri zaidi maana kwa kesho huenda ukawa umeshachelewa (1 Kor 15:24-28, 50-57).  Kwa sababu hizo, sisi tulioamini tusimame imara, na kukataa kuondoshwa kwenye hizo kweli za milele. Tunapaswa kujitoa kikamilifu kwa kazi ya bwana, na kuwaambia wengine, tukijua kwamba ingawa kazi yenyewe ni ngumu, lakini haitakuwa bure (1Kor 15:58). 

 

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili ya Watu wa Ulimwengu
Huu Ambao Bado Hawajafikiwa na Injili, Ukiwataja Kwa Majina

 

         

Afghanistan

Majina Yao

Lugha Zao

Idadi Yao

Aimaq, Jamshidi (Char Aimaq)

Aimaq, Jamshidi

92,000

Aimaq, Timuri (Teymur, Timuri)

Aimaq, Taimuri

104,000

Darwazi (Badakhshani)

Darwazi

10,000

Gawar-Bati (Narisati)

Gawar-Bati

10,000

Munji-Yidgha

Munji

10,000

                                                 


 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
for this revision and translation from the original English
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index To All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index