
1985 - 2007
4. Dondoo Za Maandalizi Ya Wokovu
Watu Unaokutana Nao Wanaweza Kuokolewa
Support Pages
Index To All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index
Kwenye Biblia Yako Soma
1 Pet 3: 8 -22; Dan 12:
2-4
Mstari Wa Kukariri
Mwe tayari sikuzote kumjibu kila
mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu;
lakini kwa upole na kwa
hofu (1 Pet 3:15)
Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Je, ni maswali gani unayoweza
kumwuliza mtu na majibu yake yakakupa wewe fursa ya kumshuhudia mtu huyo?
Mambo Ya Kufanya Kabla Hatujakutana
Tena
Hebu fikiri na ukumbuke jinsi
Bwana mwenyewe alivyokuongoza katika kumwamini, na jinsi alivyokusaidia baada
ya kumwamini. Hebu yaandike hayo mahali na kisha ufanye mazoezi ya kuwasimulia
rafiki zako mpaka uweze kufanya hivyo katika hali ya utulivu, isiyo ya kidini,
kwa muda wa dakika mbili.
Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Andika taarifa ya kurasa mbili
kuhusu ule mfano wa mwana mpotevu na jinsi unavyojifunza kuhusu watu waliopotea
na mpango wa Mungu wa kuwaokoa.
Tafakari Mstari wa Biblia Ufuatao Neno Kwa
Neno
2 Tim 1:7
Tumia
Muda wa Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu
Ombea taifa la
Ubelgiji
Wako Wazungu10,000,000; Ni Makao Makuu ya Umoja wa Ulaya;
Ni nchi yenye viwanda vingi; Wakristo waliopo ni 0.32% tu (Makanisa ya
Kiinjili)
Hakikisha umewafundisha wengine somo hili.
Kila mara
omba na kujiandaa ukiongezea mistari mingine ya Biblia
na mifano yako mwenyewe
ili kufanya somo lieleweke vizuri zaidi.
Petro, Mtume mkuu na Mchungaji mpendwa amefanya pia
kazi za Mwinjilisti mara kwa mara. Katika 1Pet 3:1-8 anaufungua moyo wake kama
mchungaji, lakini katika mstari wa 13 anawatia moyo washirika wake katika
huduma ya ushuhudiaji. Tunaenda kufuata mawaidha yake mema.
1. Ni Lazima Tuishinde Hofu
Katika nchi ya Hispania lipo kanisa la watu ambao awali waliishi mitaani. Watu hawa walikuwa wakiibia watu wengine, walitumia madawa ya kulevya na kufanya ukahaba, bila hofu yo yote. Yesu,kwa njia ya ajabu, amewaokoa kwa mamia. Walizoea kuiba hata kwenye mabenki; lakini baada ya kuokoka ukiwaambia habari ya kwenda kuwashuhudia watu wengine habari za Yesu ni ajabu kwamba wanaogopa, na kuja na hoja kama:
" Watu wanaweza kunicheka."
" Watu wanaweza kufikiria mimi nimekuwa mwendawazimu."
" Mtu anaweza kunipiga halafu. "
" Mimi sitaki kujisikia kukataliwa ujue."
Biblia inasema kwamba Mungu hakutupa sisi roho ya woga, bali roho ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi (2Tim 1:7)
Sasa
Hii Hofu Inatoka Wapi?
Je, ni nani asiyetaka sisi kuwajulisha watu habari
za Yesu? Ni Shetani. Ikiwa tutanyenyekea mbele za Mungu, tutaweza kumpinga
Shetani naye atatukimbia (Yak 4:7).
2. Ni Lazima Tukae Sawa Mioyoni Mwetu!
Ndani ya mioyo yetu ni lazima tumkubali Kristo kuwa Bwana. Kuwa chini ya Ubwana maana yake ni kuyafanya mapenzi yake; maana yake ni kufanya kila analosema ni muhimu kwake. Je, mapenzi ya Bwana wetu Yesu Kristo ni yapi?
Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kilichopotea (Lk 19:10).
Roho wa Bwana yu juu yangu, amenipaka mafuta ili niwahubirie maskini habari njema (Lk 4:18).
Je, hawaachi wale tisini na tisa na kwenda kumtafuta yule kondoo mmoja aliyepotea hadi ampate? (Lk 15:4).
Watu waliopotea na wale waliochanganyikiwa, hao ndio walio muhimu kwa Yesu. Ni kweli mtu anaweza kuponywa kutoka kwenye kitanda cha mauti, lakini ni bora zaidi kijana anapomfuata Kristo akaponywa mwili na nafsi pia. Nani ajuaye ni wangapi wanaoweza kumfuata Yesu baada yake?
3. Petro Anasema, ‘Kila Mara!’
Ni lazima tuwe tayari kuzungumza habari za Yesu wakati wote mchana na usiku. Unaweza kuwa na uhakika kwamba Mungu anaweza kuandaa mpango wa kukujaribu ili ajue uaminifu wako.
Mahali fulani kule India kikundi fulani cha wakristo waliokuwa wamechoka sana baada ya kazi ngumu katika mazingira ya joto na vumbi, walikaa kwenye mghahawa mmoja ili kujipatia riziki. Mara akatokea mhudumu Mhindu na kuanguka miguuni pao na kusema anawajua wao ni akina nani; na kisha kuwaomba wamsaidie ili aweze kumpokea Yesu. Huu haukuwa muda mzuri kwao, lakini unadhani walifanya nini? Kila mara!
4. Je, Umejiandaa?
Petro anasema ni lazima tujiandae kabla hatujaingia kwenye mapambano la sivyo ipo hatari ya kushindwa. Je, tunapaswa kujiandaa kwa namna gani? Jiandae kwa namna zifuatazo ~
Kiroho, kwa kufanya maombi.
Kibiblia, kwa kutambua moyo wa huruma wa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu.
Kwa msisimko, tutasikia habari za kusikitisha lakini tunapaswa kuwa makini katika kusikiliza, bila mshtuko bali kwa machozi.
Kwa kutumia akili, kwa sababu kuna njia nyingi za kuwapata watu mbalimbali. Je, tunazifahamu njia hizo?
Kwa vitendo, tuwe tayari kwenda wawiliwawili, tukiwa na mipango mizuri, na utaratibu mzuri wa kufuatilia, na wakati huohuo tukionesha picha nzuri.
5. Petro Anatumia Neno Hili, ‘Kila Mmoja!’
Wakati mwingine tunapata urahisi wa kuishi na baadhi ya watu, lakini tunapata ugumu kuishi na wengine. Lakini linapokuja suala la kushuhudia tunapaswa kuweka kando kila aina ya ubaguzi na upendeleo, kwa sababu kwa Yesu kila nafsi ni ya thamani; iwe ni ya mkubwa, ya mfanyakazi, au ya mtu wa hali ya chini. Mungu anapenda nafsi zote sawasawa.
6. Waruhusu Wakuulize Maswali!
Je, waweza kuanzisha mazungumzo yatakayomfanya mtu akuulize, kwa mfano, unafanya nini au kwenda wapi miisho ya wiki? Kuulizwa swali kama hilo kunakupa wewe fursa nzuri ya kusema maneno machache kuhusu imani yako au kanisa lako. Mkakati uliopo ni kuvua watu, na kumvua samaki ni lazima utumie ndoano yenye chambo. Angalia yule unayeweza kumkamata kwa uvumilivu, na huku jicho lako likiwa wazi kuona fursa zingine anazoweza kukupa Mungu.
Fursa Zaweza Kujitokeza Bila Kutazamiwa
Mchungaji mmoja aliyekuwa anasafiri kwa treni alikaa jirani na msichana ambaye baadaye alishambuliwa na pumu. Abiria wote walitazama pembeni, lakini Mchungaji yule alimwendea msichana na kumtuliza. Akasema anajua jinsi msichana huyo anavyojisikia kwa sababu yeye mwenyewe aliwahi kuugua pumu. Baadaye yule msichana alitaka kujua ni kwanini sasa haugui tena pumu. Kwa dakika chache Mchungaji yule aliweza kuelezea imani yake aliyonayo kwa Mungu anayeponya. Msichana huyo aliahidi kumtembelea Mchungaji yule.
7. Je, Unaweza Kueleza Tumaini Ulilonalo?
Unapokuwa ukizungumza na mtu mtaani na mazungumzo yenu yakabadilika na kulenga kwenye imani katika Mungu, bila shaka hutachukua zaidi ya dakika mbili kumweleza ni nini Yesu alichokufanyia. Je unaweza kufanya hivyo? Kwanini usifanye mazoezi na rafiki zako? Kila mmoja atafanya zoezi la kumshuhudia mwenzake kwa zamu.
8. Chunga Sana Msimamo Wako
Msimamo wako na tabasamu lako vyaweza kusema kwa sauti kubwa kuliko maneno. Petro anasema kwamba tunapaswa kusema kwa upole na adabu. Sifa hizi ni adimu sana katika ulimwengu tunamoishi sasa.
9. Hatimaye Uwe Tayari Kuteseka
Petro anasema kwamba, ikiwa ni mapenzi ya Mungu, uwe tayari kuteseka kwa kufanya mema. Baadhi ya watu hawatataka kukusikiliza. Usijali hata kama watakucheka au kukutukana. Yote ni juu ya Yesu aliyefia dhambi mara moja tu,mwenye haki kwa ajili ya wasio haki; huyo atakuleta kwa Mungu.
Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa
Ulimwengu
Huu Ambao Bado Hawajafikiwa Na Injili; Wataje Kwa Majina
|
Algeria |
||
|
Jina La Watu |
Lugha Yao |
Idadi Yao |
|
Hoggar, Ahaggaren |
Tamahaq, Hoggar |
31,000 |

1985 - 2007
With many thanks to Pastor Dastan
Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
for this revision and translation from the original English
mboeradsk @ yahoo.com
© Dr Les Norman The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide
copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial
purposes. Freely you have received, so please freely give.
Support Pages
Index To All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index