
1985 - 2007
5. Mtindo
wa Maisha wa Mwinjilisti
Je, ni kitu gani
kinachowafanya watu wasikilize?
Support Pages
Index To All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index
Katika Biblia Yako Soma
Marko 1
Mstari
wa Kukariri
(Yesu) akasema, "Wakati
umetimia, na Ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili” (Mk 1:15).
Baadaye
Zungumzieni Jambo Hili
Peaneni changamoto kwa kuulizana
maswali yaliyoko mwishoni mwa somo
Jambo
la Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Ni wakati wa kutenda yale
Yesu aliyotenda, kwa kwenda katika kijiji ambacho hujawahi kufika na kuhubiri
huko. Baada ya maombi nendeni wawiliwawili, au kama kikundi kwa pamoja.
Kazi
ya Kuandika Ya Stashahada
Pitia vitabu vya Injili na
Waebrania 5:7 kisha andika ukurasa mmoja ukielezea maisha ya Yesu kimaombi.
Tafakari
Mistari Hii Neno Kwa Neno
Waebrania 2:3,4
Tumia Dakika Moja Kuubadilisha
Ulimwengu
Ombea taifa la Mongolia
Idadi ya watu: 3,000,000
Waamini wanaweza kuwa ni 1,000 tu
Kuna mateso mengi na unyonyaji
Hakikisha umewafundisha wengine somo hili.
Kila mara
omba na kujiandaa ukiongezea mistari mingine ya Biblia
na mifano yako mwenyewe
ili kufanya somo lieleweke vizuri zaidi.
Marko 1:45 inatuambia
kwamba watu walikuja kwa Yesu kutoka kila mahali. Watu hao hawakuja kanisani,
wala kwenye mikutano ya Injili, wala kwenye umisheni au kazi nyingine. Walikuja
kwa Yesu. Kama tukiweza kugundua ni kwa nini walikuja, na tukafanya kama
alivyofanya Yesu, watu wataendelea kuja kwa Yesu hata sasa kutoka pande zote.
1. Yesu Alimkaribisha Roho Mtakatifu
Yesu alimsikiliza Roho Mtakatifu, (Mk 1:9-12), alitii na kujiachia Yeye na huduma yake kwa uongozi wa Roho, akienda na kutenda sawasawa na maelekezo ya Roho.
Kwanini
Jambo Hili Ni Muhimu Kiasi Hicho?
Yesu alikuwa, na hata sasa
ni Mungu, lakini alipozaliwa aliamua kuacha uweza wake wa kimbingu (Flp 2:6,7).
Alichagua kuja kama mtoto mchanga wa kawaida ya kibinadamu, na sio kama
jemadari, au mfanyabiashara tajiri, au mtawala mwanasiasa. Yesu aliishi kama
mwanadamu wa kawaida; na kama sisi alihisi baridi, njaa, kiu, furaha na huzuni.
Alihudumu pia kama mwanadamu wa kawaida, lakini kama mwanadamu aliyepewa uweza
na Roho Mtakatifu. Vivyo hivyo sisi nasi tunaweza na tunapaswa kuhudumu katika
uweza wa Roho Mtakatifu
(Lk 4:18).
2. Yesu Alishinda Majaribu Ya Shetani
Kule nyikani Yesu alikuwa dhaifu na mwenye njaa wakati Shetani alipomjaribu ili atumie vibaya uweza wake kubadilisha mawe kuwa mkate. Tena Shetani alimjaribu ili akwepe mateso ya Msalaba, na kisha tena akamjaribu ili ajikweze, lakini kila mara Yesu alimkatalia Shetani na akachagua kuwa mwaminifu kwa Mungu na kwa kusudi lake. Shetani aliondoka zake akiwa ameshindwa (Mk 1:13) (Mt 4:1-11).
3. Yesu Aliyapa Mahubiri Kipaumbele
Alisema ujumbe wake ni habari njema.
Alisema ufalme wa Mungu umekaribia.
Alisema wakati umewadia.
Aliwataka watu watubu na kuamini (Mk 1:14).
Mara kadhaa tunashuhudia habari za Yesu kimyakimya na kwa upendo kupitia maisha yetu, lakini hatimaye inabidi watu wapewe changamoto ya kutubu, wamgeukie Mungu na kutubu, au la. Asije mtu akasema kwamba kuhubiri si muhimu. Miguel Diez alikuwa na wasikilizaji 3,000 katika mkutano wa hadhara huko Ecuador, Pensacola. Kanisa huko Florida limeshuhudia waamini wapya 100,000 katika kipindi cha miaka miwili; na Carlos Anacondia wa Argentina ameshuhudia zaidi ya watu 8,000,000 wakimpokea Kristo kupitia mahubiri.
4. Yesu Aliujua Wakati Wa Mungu
Yesu alifanya kazi hadi alipofikia miaka thelathini lakini Herode alipomweka Yohana gerezani, hiyo ilikuwa ni ishara ya Mungu. Yesu alijua wakati wake umewadia. Tunaambiwa tukeshe, ili tupate kujua ni wakati gani Yesu yuko mlangoni. Kama tukiangalia kwa jicho moja neno la Mungu la unabii, na kanisa, na Israeli; na jicho lingine tukaangalia matukio ya ulimwengu, tutazijua nyakati (Mk 13:28-36) (Mt 16:1-3).
Nuhu alizijua nyakati, akajenga safina.
Musa alizijua nyakati, akaongoza watu wa Mungu kutoka utumwani.
Danieli alizijua nyakati, akaomba ili kwamba watu wa Mungu waliopelekwa utumwani wapate kuachiliwa.
Mungu aliujua wakati, akamtuma Yesu.
Yesu aliujua wakati, akahubiri.
5. Yesu Aliwaita Wengine Ili Wamsaidie
Hakufanya kila kitu peke yake (Mk 1:16-20). Watu waliusikia mwito wa Kristo na kutii bila kukawia, wakaacha kila kitu na kumfuata Yesu, hivyo kwamba mashahidi waliongezeka na kushirikiana kufanya kazi iliyokuwa mbele yao.
Kwanza alikuwako Yesu peke yake.
Kisha, Yesu na wale Thenashara.
Halafu, ikawa ni wale Thenashara na wengine 3,000 zaidi.
Halafu 3,000 wakawa Wayahudi 5,000.
Kisha watu kutoka mataifa mengine wakajiunga.
Hatimaye Injili ikafika Afrika na Asia, na kuendelea.
6. Yesu Alidhihirisha Uweza Wa Mungu
Alimtoa pepo (Mk 1:25).
Aliponya mwenye homa (Mk 1:31).
Aliponya wengi na kutoa mapepo (Mk 1:33,39).
Alimponya mwenye ukoma (Mk 1:42).
Kila wakati Yesu alipoonesha uweza wa Mungu ambao
ni upendo na huruma ya Mungu ikifanya kazi, habari zilienea (Mk 1:28,45), kiasi
kwamba mji wote ulikuja kumwona (Mk 1:33,37).
7. Yesu Aliomba Kwa Dhati
Yesu alitenda
kazi alizoona Baba yake akitenda (Yn 5:19), na ili aweze kutenda kazi hizo,
alitenga muda wa kumsikiliza Baba yake. Wakati mwingine ilikuwa ni alfajiri au
usiku wa manane au usiku mzima; akiwa faraghani au hadharani. Hatimaye alijua ni nini la kufanya
(Mk
1:35).
8. Yesu Alijitoa Kwa Watu
Alikuwa na fursa ya kukaa mahali pamoja na kujulikana, lakini Yesu alitaka kwenda hata vijiji vya jirani ili ahubiri huko pia (Mk 1:37-39). Yesu alipenda watu, hata wale wasiopendeka kama vile wenye mapepo wachafu, yule mwanamke mgonjwa, na wenye ukoma. Kwa Yesu lilikuwa ni suala la kujitoa ili kuwafikia watu wengi zaidi na upendo wa Mungu. Matokeo yake ni kwamba watu wengi walimjia kutoka kila mahali, na bado wanaendelea kumjia.
Yesu alikuwa ni mwanadamu katika uweza wa Roho Mtakatifu. Yesu akasema kwamba ye yote atakayemwamini atatenda si hayo tu, ila na yaliyo makubwa zaidi kwa uweza wa Roho Mtakatifu yuleyule ambaye Yesu alimtuma kwetu.
9. Maswali Ya Kujiuliza
Je, una mipango gani ya kuwafikia watu?
Je, unajitoaje kwa ajili ya maombi?
Je, unatumia karama za Roho?
Je, unaitikia wito wa Yesu?
Je,waweza kuona kwamba wakati wa Mungu ni sasa?
Je, kuhubiri umekupa umuhimu wa kwanza?
Je, unashinda majaribu ya Shetani kila siku kwa maombi, kwa neno na kufanya maamuzi matakatifu?
Je, ulimpokea Roho Mtakatifu siku ulipoamini, na je, unaendelea kujazwa Naye kila siku?
Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa
Ulimwengu
Huu Ambao Bado Hawajafikiwa Na Injili; Wataje Kwa Majina
|
Azerbaijan |
||
|
Jina la Watu |
Lugha Yao |
Idadi Yao |
|
Avar |
Avar |
46,000 |
|
Tat, Mussulman |
Tat, Mussulman |
22,000 |
|
Tatar |
Tatar |
29,000 |
|
Turk |
Turkish |
19,000 |

1985 - 2007
With many thanks to Pastor Dastan
Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
for this revision and translation from the original English
mboeradsk @ yahoo.com
© Dr Les Norman The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide
copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial
purposes. Freely you have received, so please freely give.
Support Pages
Index To All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index