
1985 - 2007
6. Kwa Vyo
Vyote Vile
Kuwashuhudia
jamaa zetu na rafiki zetu kunahitaji uinjilisti wa nguvu
Support Pages
Index To All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index
Katika Biblia Yako Soma
Mithali 24
Mstari wa Kukariri
“Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia.” ( Warumi 1:16).
Baadaye Zungumzia Jambo Hili
Je, yaliyomo katika aya ya
kwanza ni ya kweli? Kama ni kweli, je,
tunaamini yale anayosema mwandishi, na tunakwenda kufanya nini?
Jambo la Kufanya Kabla Hatujakutana
Tena
Hebu andaa orodha wa jamaa yako na
wale wanaohusiana na wewe kwa karibu kama vile wazazi, mababu, watoto,
mashangazi, mabinamu, wapwa; wale tu walio hai. Watembelee angalao watano, na
uwaambie kile unachokifanya. Wasikilize na tazama. Je, Baba anamvuta ye yote?
Kazi ya Kuandika Ya Stashahada
Tazama orodha iliyoko katika aya
ya pili. Ni mtu wa namna gani anaweza kusema, “Ukristo? Kamwe sijawahi kusikia”
Yawezekana ni mwanakijiji wa ndani kabisa huko Uchina ambaye hajawahi kuguswa
kabisa na Injili au kupitiwa na mmishenari. Andika taarifa ya aya moja
ukimwelezea jinsi alivyo na sababu zinazoweza kumfanya aseme hivyo. Kwa kutumia
uwezo wako wa kubuni andika aya nyingine ukielezea ni nani wanaoweza kutoa yale
majibu mengine kumi na kwanini.
Tafakari Mistari Hii ya Biblia Neno Kwa
Neno
Rum 10:14,15
Tumia Muda Mfupi
Kuubadilisha Ulimwengu
Omba Kwa Ajili ya
Misri
Idadi ya Watu: 60,000,000
Waislamu ni 86%, Orthodox ni 13%
Kanisa Linateswa
Hakikisha umewafundisha wengine somo hili.
Kila mara
omba na kujiandaa ukiongezea mistari mingine ya Biblia
na mifano yako mwenyewe
ili kufanya somo lieleweke vizuri zaidi.
Sisi binadamu tunayo namna ya kuwagawa watu
katika makundi mabalimbali; weupe na weusi, tajiri na maskini, wasomi na wasio
wasomi, wenyeji na wageni n.k. Lakini Yesu aliwagawa wanadamu katika makundi
mawili tu; waliookoka na ambao bado hawajaokoka, waliozaliwa mara ya pili na
ambao bado. Mstari huu aliouchora Yesu
unawafanya watu waishi upande mmojawapo, wengine upande huu na wengine upande
huu (Stanley Jones, wa India).
1. Ni Nini Mapenzi Ya Mungu?
Bwana ni mvumilivu, hataki hata mmoja aangamie, bali kila mmoja afikie toba. Na hekima ya Mungu katika jambo hili ni kutufaya sisi kuwa watendakazi pamoja naye. Sisi ni mwili wa Kristo; mikono yake, miguu yake, na mdomo wake hapa duniani.(2 Pet 3:9).
2. Mwanadamu Yuko Wapi?
Mtu anaweza kuwa anaishi kijijini ndani kabisa; na mwingine akawa anaishi mjini na maisha ya kisasa kabisa. Usije ukadhani kwamba yule anayeishi kijijini ndiye asiyemjua Mungu kabisa, na kwamba yule wa mjini ndiye aliye nafuu. Watu wote wapo katika hatua tofauti-tofauti za kuiamini Injili. Kwahiyo ni muhimu kuweza kugundua mwanadamu aliko katika hizo hatua mbalimbali ili uweze kujua ni nini neno jema la kumwambia.
Ukristo? Kamwe sijapata kuusikia.
Ukristo? Ndiyo, nimewahi kuusikia, lakini ni kitu gani basi?
Nimesikia Injili.
Nimeielewa Injili.
Injili ni muhimu kwangu.
Ninahitaji msamaha wa Mungu na upendo wake.
Nipe changamoto kumpokea Kristo.
Omba pamoja nami ili nimpokee Kristo.
Bado ninatafakari uamuzi nilioufanya.
Ndiyo, nataka kujiunga na kanisa.
Ndiyo, nataka kuwaeleza wengine.
3. Yatupasa Kufanya Nini?
Paulo ni mfano mzuri wa kuigwa. Kwa Wayahudi alijifanya kuwa Myahudi, kwa Mataifa naye alijifanya kuwa Mmataifa, na kwa walio dhaifu naye alijifanya dhaifu, ili kwamba kwa vyo vyote iwezekanavyo aweze kuwaokoa. Huo ndio uinjilisti, (1 Kor 9:19-23).Iwapo kanisa litaanza kuishi maisha ya ubinafsi, badala ya kuishi kwa ajili ya wale walioko nje, basi huo waweza kuwa mwanzo kifo cha taratibu cha kanisa hilo. Uinjilisti ni msisimko na damu ya uhai kwa kanisa. Kila mshirika hana budi kuwa shahidi, kila siku.
4. Uinjilisti Wa Mtu Kwa Mtu
Waamini wengi wapo tayari, lakini waanzie wapi?
Yesu alisema waende wawili wawili, sio mtu peke yake; na aende na rafiki wa jinsia moja naye.
Namna bora ya kujifunza uinjilisti ni kufanya kwa vitendo; kwanza shirikiana na wengine katika zoezi hilo ukiwa msaidizi.
Anza kushughulika na jamaa yako na rafiki zako; watu unaowaona mara kwa mara na ambao wanakufahamu vizuri. Bila shaka wameona mabadiliko fulani katika maisha yako na wamebaki kushangaa, hawaelewi kinachoendelea.
Uwe na imani kwa ajili ya jamaa yako na rafiki zako kwani kwa kuwa hawajaamini hawana imani wao wenyewe. Waazime ya kwako, amini kwa niaba yao.
Mwombe Roho Mtakatifu atamalaki.
Kila mara zungumza habari za Yesu. Sema kwamba anaponya, anabariki na kusamehe dhambi leo. Hata sasa yupo hapa tayari kusaidia. Uwe tayari kufanya maombi na watu ili kuona Bwana atafanya nini.
Onesha upendo wa Mungu kwa utayari wako wa kusaidia kwa vitendo.(1 Yoh 3:18).
Omba kwa ajili ya jamaa mbalimbali kwa kuwa hayo ndiyo mapenzi ya Mungu. Ruhusu watu wajadili na jamaa zao suala la kumfuata Yesu. Yawezekana wote wakawa tayari kumfuata Yesu; hata hivyo iwapo baadhi watapinga, huo upinzani utasaidia kuwafanya wale waliokubali kufanya uamuzi wa dhati.(Mdo 16:31).
5. Je, Utajuaje Mtu Wa Kumshuhudia?
Siri ni kuona kile Mungu anachofanya nawe ujiunge kufanya hicho hicho. Je, utafanyaje? Katika Warumi 3:10 Biblia inatuambia kwamba hakuna mtu anayemtafuta Mungu, na Yesu akasema katika Yohana 6:44 kwamba hakuna mtu anayeweza kumwendea Yesu asipokuwa amevutwa na Baba.
Je, waweza
kuona dalili yo yote ya Mungu akitenda kazi?
Tunaweza kuelewa jambo hili kwamba
tunapomwona mwenye dhambi anaonesha nia ya kumpokea Yesu ni kwa sababu amevutwa
na Baba. Kwahiyo ukiona dalili kidogo tu, acha kila kitu na kujiunga na Mungu
katika kazi anayoifanya. Hii ndiyo namna ya kuweza kujua anachokifanya Baba.
Hakuna sababu ya kukimbizana na watu mitaani, watu ambao hawaoneshi nia ya
kumpokea Yesu sasa. Hao waache mikononi mwa Mungu mwenyewe, anajua wakati
wao.(Mt 10:14).
6. Kanisa Linawezaje Kueneza Injili?
Kwa ujumla kuna njia tatu, lakini kila mara omba na kumwamini Mungu katika uongozi wake.
Maisha
Yaliyobadilishwa
Huu ni ushuhuda wa maisha
yaliyobadilishwa na ubora unaotolewa na Kristo. Ila uhakikishe kwamba
washirika ni wakristo wa kweli kwa sababu watu wanaweza kuona tabia isiyokuwa
nzuri na kuikataa Injili. Maisha yetu yanaweza kuwa ni Biblia pekee ambayo
baadhi ya watu wamewahi kuisoma. Shughuli za kijamii kama kuwasaidia maskini,
wenye njaa, wagonjwa na wafungwa, ni ushuhudiaji wenye nguvu.
Uinjilisti
wa Kutangaza
Huu ni uinjilisti ambapo Injili
inatangazwa na kuwaleta watu mahali pa kufanya uamuzi. Hii inatekelezwa kwa
kuhubiri, kushuhudia mitaani, kampeni, kugawa vipeperushi, na kuonesha sinema.
Uinjilisti
wa Kushawishi
Katika 2 Kor 5:11 Paulo
anazungumzia habari ya kushawishi watu. Makanisa mengine wanatekeleza jambo hili
kwa kuwa na vipindi vya kujifunza Biblia, kufanya mazungumzo katika jumuiya
mbalimbali k.v. vyuo vikuu, na hata majumbani. Wakati mwingine wanatumia redio
na runinga. Wanawatembelea watu majumbani mwao mara kwa mara ili kuwashawishi
watu wamkubali Kristo. Wengine huwaandaa washirika wao na kuwatuma kufanya
uinjilisti kama alivyofanya Paulo. (Mdo 19:8).
Zaidi ya yote ni kwamba, kila aina ya uinjilisti inakuwa na matokeo mazuri kwa kutegemea maisha ya maombi. Yafaa sana kuzungumza na Mungu kuhusu watu kabla ya kuzungumza na watu kuhusu Mungu..
Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa
Ulimwengu
Huu Ambao Bado Hawajafikiwa Na Injili; Wataje Kwa Majina
|
Bangladesh |
||
|
Jina la Watu |
Lugha Yao |
Idadi Yao |
|
Burmese |
Burmese |
100,000 |
|
Gujarati |
Gujarati |
66,000 |
|
Nepalese |
Nepali |
17,000 |
|
Orisi (Utkali, Vadiya) |
Oriya |
13,300 |

1985 - 2007
With many thanks to Pastor Dastan
Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
for this revision and translation from the original English
mboeradsk @ yahoo.com
© Dr Les Norman The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide
copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial
purposes. Freely you have received, so please freely give.
Support Pages
Index To All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index