
1985 - 2007
7. Kuwezeshwa
Neno la Mungu, Roho wa Mungu, na watu wa Mungu wapo ili kukusaidia
Support Pages
Index To All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index
Katika Biblia Yako Soma
(2 Tim 3:14-17) (Lk 4:18) (Ebr
12:1-3).
Mstari wa Kukariri
Hata twathubutu kusema, Bwana
ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini? (Ebr 13:6).
Baadaye Zungumzia Jambo Hili
Ikiwa sasa umejua jinsi Mungu
anavyopanga kukutegemeza, kwanini usizungumze tu habari za Yesu?
Jambo La Kufanya Kabla
Hatujakutana Tena
Andaa kunena habari za Yesu na mtu
mmoja, au kikundi kidogo, au kanisa , na azimia kupanda mbegu za neno la Mungu.
Tafuta fursa nzuri na mruhusu Roho wa Mungu afanye kazi, na waambie hao
wasikilizaji wako habari za watu wa maana katika jamaa ya Mungu, wa zama za
kale au wa zama hizi.
Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Andika kurasa mbili za muhtasari
wa ujumbe wako na umkabidhi mwalimu kwa masahihisho.
Tafakari Mistari Hii Ya Biblia
Neno Kwa Neno
1 Kor 9: 15-18
Tumia
Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu
Omba kwa ajili ya
India
Idadi ya watu: 900,000,000 (Wahindu/Waislamu)
Ukristo unakua kwa kasi sasa; lakini wengi na ambao ni maskini hawajafikiwa
Hakikisha umewafundisha wengine somo hili.
Kila mara
omba na kujiandaa ukiongezea mistari mingine ya Biblia
na mifano yako mwenyewe
ili kufanya somo lieleweke vizuri zaidi.
Tunakwenda kuzungumza kuhusu njia tatu
ambapo Mungu hukutegemeza unapowashuhudia watu habari za Yesu mkiwa faragha au
hadharani. Anakutegemeza kwa nguvu ya Neno lake, kwa nguvu ya Roho wake, na kwa
ushuhuda wenye nguvu wa watu wake.
1. Uweza Wa Neno Lake
Neno la Mungu ni la kipekee tofauti na neno la mwanadamu kwa sababu Neno la Mungu ~
Li hai - Ebr 4:12, 1 Pet 1:23, Mdo 7:38
Linakuandaa - 2Tim 3:16
Linatimiliza kazi - Isa 55:11
Ni kama nyundo inayopasua miamba - Yer 23:29
Linafanya kazi ndani ya watu - 1The 2:13
Ni upanga anaoutumia Roho wa Mungu - Efe 6:17
Ni kama mbegu iliyopandwa - Mk 4:13-20
· Shetani hutwaa baadhi ya mbegu.
· Wengine hawaipi nafasi kuota.
· Wengine huruhusu hofu na kutokupanda mbegu.
Bali wengi wanaolisikia Neno wanafananishwa na udongo mzuri, na hilo Neno huwawezesha kuzaa wengine mara 30, wengine mara 60, na wengine mara 100. Wewe wajua kwamba sehemu kubwa ya shamba ni udongo mzuri, sehemu ndogo ni mawe na magugu yanaota pembeni; kwahiyo tazamia watu wengi kukua katika kweli. Yesu anasema mbegu hiyo hukua yenyewe, bila kuonekana, kidogokidogo hadi wakati wa mavuno. Kwahiyo mkulima mzuri hupanda na kusubiri kwa saburi na matumaini (Mk 4:26-29).
2. Uweza Wa Roho Wa Mungu
Atafuatilia ushuhuda wako kwa ishara kuu kutoka kwa Mungu kwa kadiri unavyoendelea kuomba kwa ajili ya watu wenye uhitaji. Ishara huelekeza njia ya kuingia kwenye Ufalme wa Mungu ambako watakutana na upendo na ulinzi wake.
Je,
Tutazamie Kuona Ishara Gani?
Akinukuu Isa 61:1,2 Yesu anasema
katika Lk 4:18 kwamba Injili itakapohubiriwa kwa maskini:
Waliovunjika mioyo wataponywa.
Wafungwa watafunguliwa.
Vipofu watapata kuona.
Waliosetwa wataachiliwa huru.
Upendeleo waweza bado kupatikana kwa Bwana.
Siku moja Yohana Mbatizaji, alipokuwa gerezani na akiwa amekata tamaa, kwa kutokuona uwezo wa Mungu licha ya kwamba aliihubiri kweli Yake, alituma ujumbe kwa Yesu akitaka kujua kama Yeye ndiye Masihi mwenyewe au la! Yesu alisema ishara zifuatazo zinamwelekezea Yeye:
Wagonjwa wanaponywa..
Mapepo wachafu wanatolewa.
Viwete wanatembea.
Wakoma wanatakaswa.
Viziwi wanapata kusikia.
Wafu wanafufuliwa.
(Angalia Yn 10:41, Lk 7:20-23)
Siku hizi wakristo wanaona ishara kila mahali hapa duniani. Yesu atakufanya nawe uone ishara utakapowaombea watu kwa Jina lake. Kwahiyo tunaweza kuongezea orodha yetu ishara alizoahidi Yesu katika Mk 16:17-20.
Kunena kwa lugha. (Moja ya karama za Roho Mtakatifu)
Ulinzi dhidi ya hatari.
Ishara zinazolithibitisha Neno.
Tufanye nini sasa?
Iga mfano wa Yesu katika Mdo 10:38.
Mwamini Yesu katika ahadi zake kwetu.(Mdo 1:8,Yn 14:12).
Iga mfano wa kanisa la kwanza; wao walihubiri Neno na kutembea katika uwezo wa Roho wa Mungu mara kwa mara. Soma kitabu cha Matendo ya Mitume.
3. Ushuhuda Wa Watu Wa Mungu
Licha ya unafiki wa wasioamini na tuhuma zao dhidi ya kanisa(wakati mwingine tuhuma hizo ni za kweli, waweza kuomba radhi), lakini waweza kuja na uthibitisho wa maisha yaliyobadilishwa, na hasa yako mwenyewe.
Unaweza kutoa ushuhuda wa upendo unaoonekana miongoni mwa watoto wa Mungu; unaweza kusimulia kuhusu maisha wa watoto wa Mungu kutoka kwenye Biblia, na wale wanaoishi katika siku zetu. Utagundua kwamba watu watawaheshimu watu mashuhuri wa Mungu, lakini watawadharau na kuwabeza wale walio vuguvugu.
Unaweza kuwataja watu mashuhuri waliofanya Matengenezo ya Kanisa;
Unaweza kusimulia habari za maisha ya watu mashuhuri kama William Wilberforce, mkristo aliyekomesha utumwa;
Shaftesbury, aliyewapigania maskini; Dr. Barnardo, aliyewasaidia yatima;
Booth, aliyeanzisha Jeshi la Wokovu;
Askofu Tutu, aliyepinga ubaguzi wa rangi.
Wataje watu mashuhuri walioleta ustaarabu, kama
Mmishenari Livingstone, Studd, walioishi na kufia Afrika;
Taylor, aliyeishi na kufia China;
Carey, aliyeishi na kufia India;
Judson, aliyeishi na kufia Burma;
Billy Graham, anayewahubiria mamilioni ya watu.
Wataje ‘Wasamaria Wema’.
Linapojitokeza suala la kuwasaidia wenye njaa, walio na kiu, wagonjwa, wasio na makazi, na wafungwa, watu wa Mungu wapo tayari. Wakristo ulimwengu mzima wanafanya kazi kwa bidii ili kuonesha upendo wa Mungu, ama kwa malipo kidogo au kwa kujitolea.
Shirika la ACET huwajali waathirika wa UKIMWI;
Remar, hujishughulisha na matatizo ya vijana, na
Jackie Pullinger anapambana na madawa ya kulevya;
Mama Teresa wa Calcutta alijishughulisha na wagonjwa na wanaokufa.
Kanisa katika nchi za Afrika Kusini, Romania, Poland, na Latin America
Linapinga dhuluma kwa nguvu kubwa.
Wakristo katika nchi za Magharibi wanapiga vita utoaji mimba na maovu mengine ya kijamii.
Ukiachilia mbali kushindwa na kuanguka kwa hapa na pale, lakini bado Wakristo wanatembea kifua mbele kama wakitahiniwa kwa haki, mahali po pote, na wakati wo wote. Baada ya miaka ipatayo 2000 ya mashambulizi na mateso, watu wa Mungu bado wako hai na idadi yao inaongezeka kwa kasi kubwa ulimwenguni kote. Kwa kutegemezwa na Neno lililo hai la Mungu, uweza wa Roho wa Mungu, na upendo na huruma ya watu wa Mungu, tunatazamia kuendelea kukua hadi Yesu atakaporudi tena.
Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa
Ulimwengu
Huu Ambao Bado Hawajafikiwa Na Injili; Wataje Kwa Majina
|
Ubelgiji |
||
|
Jina La Watu |
Lugha Yao |
Idadi Yao |
|
Kurd, Northern (Kermanji) |
Kermanji (Kurmanji) |
13,000 |

1985 - 2007
With many thanks to Pastor Dastan
Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
for this revision and translation from the original English
mboeradsk @ yahoo.com
© Dr Les Norman The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide
copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial
purposes. Freely you have received, so please freely give.
Support Pages
Index To All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index